TAA YAWALIPA FIDIA YA VIWANJA WANANCHI WA KIPUNGUNI A

3-minMAMLAKA ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) kwa kushirikiana na Ofisi ya Manispaa ya Ilala,Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ilala na Kampuni ya Tanzania Remix  imeanza kutekeleza agizo la Naibu Waziri Ujenzi uchukuzi na Mawasiliano (Uchukuzi)  Mhandisi Atashasta Nditiye juu ya ulipaji wa fidia ya Viwanja kwa Wananchi wa Kata ya kipunguni A na Kipunguni mashariki.

Agizo hilo alilotoa Agosti 30 mwaka huu limeanza kutekelezwa leo  kwa Wananchi watokao Kipunguni Mashariki na Kipunguni A kwenda  mtaa wa Kidole na Luhanga kupewa viwanja 537 ndani ya kata ya Msongola ili kupisha mradi wa upanuzi wa kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius  Nyerere(JNIA).

Awali Mhandisi Nditiye alitoa maagizo kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege  Bw, Richard Mayongela kushirikiana na Manispaa ya Ilala ,Mkuu wa Wilaya na Kampuni ya Tanzania Remix ambayo ilihusika na upimaji wa maeneo hayo kuhakikisha inawagawia Wananchi viwanja hivyo na kuhakikisha viwanja hivyo vina ubora.

“Mshirikiane na Tanzania Remix na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya na Manispaa kuwagawia Wananchi viwanja hivi vilevile  shirikianeni na  vyombo vya ulinzi na usalama kuwabaini  wafanyakazi wote wa TAA waliojiingiza kwenye mradi huu na kujipatia viwanja kinyume na utaratibu angali hawakuguswa na mradi huu wabainishwe na wachukuliwe hatua kali za kisheria”alisema.

Safari Kishiwa na Evaline Malume ni miongoni mwa Wananchi walioanza kugawiwa viwanja hivyo nakuishukuru Serikali kutokana na maeneo hayo kuwa katika mazingira mazuri.

Wananchi hao walidai wanawashangaa baadhi ya wananchi wenzao walioathiriwa na mradi huo kukimbilia mahakamani kwasababu mbalimbali  zisizo na mashiko.

"Tuwaombe tu wenzetu wafute kesi waje wachukue viwanja viwanja hivi vipo kwenye mazingira mazuri tofauti na wanavyofikiri"walisema.

Contact Us

Tel (Gen): +255 22 2842402/3
Fax: +255 22 2844495
Email: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.
P.O.Box 18000 Dar Es Salaam

Feedback & Enquires