KOICA Yaendesha Mafunzo Kuwajengea Uwezo Wafanyakazi wa TAA

Watendaji wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) kutoka Menejimenti na Vitengo vya Usalama, na uzuiaji wa wanyama pori na ndege hai leo wameshiriki katika mafunzo ya kuwajengea uwezo wa utendaji katika Viwanja vya Ndege yaliyoandaliwa na KOICA (Korea International Cooperation Agency) na kutekelezwa na wataalam kutoka Kiwanja cha Ndege cha Incheon kilichopo Korea Kusini ambacho kinaaminika kuwa na ubora nambari moja katika nyanja ya usalama na uendeshaji duniani.

Mafunzo hayo yamefanyika katika Ukumbi wa watu mashuhuri Katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere Jengo la pili la abiria (TB II), ikiwa ni mwendelezo wa mpango wa mafunzo ya miaka mitatu kwa watendaji wa TAA na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Zanzibar (ZAA).

Akitoa maelezo kuhusu mafunzo hayo Meneja wa Mafunzo kutoka Kiwanja cha Ndege cha Incheon Bi. Ji-Yoon Park ameeleza kwamba mafunzo hayo ni mwendelezo wa mafunzo ya awali ambapo kwa awamu ya kwanza Mafunzo yalitolewa kwa watendaji takribani 15 kutoka TAA na ZAA na mafunzo haya ni sehemu ya mpango wa mafunzo ya miaka mitatu (2018 – 2020).

Mafunzo haya yatafanyika kwa siku mbili kuanzia leo tarehe 15 Aprili na yatamalizika siku ya kesho16 Aprili nakuendelea huko Zanzibar ambapo yatafanyika katika Mamlaka ya Viwanja vya ndege Zanzibar.

Katika awamu ya kwanza ya mafunzo haya yalifanyika mwezi Septemba mwaka jana na Watendaji kumi na tano (15) walinufaika na mafunzo haya ikiwa ni (10) kutoka TAA na watendaji na watano (05) kutoka ZAA.

Ikumbukwe kuwa TAA na ZAA mnamo Juni 2018 waliingia katika makubaliano na KOICA ya kutoa mafunzo kwa Watumishi kwa muda wa miaka mitatu ambapo kufikia mwaka 2020 Watumishi 45 watakuwa wamenufaika na mafunzo hayo kutoka Utawala, kada za Ulinzi na Usalama, Tehama, na Uendeshaji.

Contact Us

Tel (Gen): +255 22 2842402/3
Fax: +255 22 2844495
Email: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.
P.O.Box 18000 Dar Es Salaam

Feedback & Enquires