Tanzania Airports Authority Blog

  • Home
    Home This is where you can find all the blog posts throughout the site.
Site Admin

Site Admin

Super User has not set their biography yet

jpm-1

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na viongozi mbalimbali akikata utepe kuashiria kufungua rasmi Jengo la Tatu la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo Alhamisi Agosti 1, 2019

 

jpm-2

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Viongozi wa Dini, Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubeiry bin Ally na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Katoliki la Dar es Salaam Muadhama Polycarp Kardinali Pengo na viongozi wengine wakifunua pazia kama ishara ya ufunguzi rasmi wa Jengo la Tatu la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam leo Alhamisi Agosti 1, 2019.

 

jpm-3

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli (aliyenoosha kidole) wakati wakipata maelezo mbalimbali kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), ,Mhandisi Julius Ndyamukama (kulia) mara baada ya kuzindua rasmi Jengo la Tatu la Abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere, leo Agosti 1, 2019.

 

jpm-4

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Wafanyakazi wa Benki ya NMB, ambao wanatoa huduma ya kubadilisha fedha ndani ya Jengo la Tatu la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere, ambalo amezindulia leo Agosti 1, 2019.

 

Hits: 149
0

DSC 6549-min

Watendaji wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) kutoka Menejimenti na Vitengo vya Usalama, Uendeshaji na uzuiaji wanyamapori wakiwa katika mafunzo ndani ya Ukumbi wa watu Mashuhuri (VIP) katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA TB II).Walioketi mbele kushoto ni Meneja Rasilimali watu na Utawala Bw. Abdi Mkwizu kulia ni Mkurugenzi wa kituo cha Mafunzo ya Anga cha Kiwanja cha Ndege cha Incheon Bw. Chin Hyong, Ryu.

 

DSC 6544-min

Msimamizi Mwandamizi na Mkaguzi wa Usalama wa anga Bw. Sanghoom (Mark) Lim akitoa mafunzo kwa Watendaji wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) kutoka Menejimenti na Vitengo vya Usalama, Uendeshaji na uzuiaji wanyamapori kuhusu masuala ya Usalama katika Viwanja vya Ndege ndani ya Ukumbi wa watu Mashuhuri (VIP) katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA TB II).

 

DSC 6573-min

Meneja wa Mafunzo kutoka Kiwanja cha Ndege cha Incheoni Bi. Ji-Yoon Park akitoa mafunzo kwa Watendaji wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) kutoka Menejimenti na Vitengo vya Usalama, Uendeshaji na uzuiaji wanyamapori kuhusu namna ya kuandaa mpango wa kuwaongezea uwezo watendaji katika Viwanja vya Ndege. Mafunzo hayo yamefanyika ndani ya Ukumbi wa watu Mashuhuri (VIP) katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA TB).

Hits: 2072
0

Contact Us

Tel (Gen): +255 22 2842402/3
Fax: +255 22 2844495
Email: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.
P.O.Box 18000 Dar Es Salaam

Feedback & Enquires