Tanzania Airports Authority Blog

  • Home
    Home This is where you can find all the blog posts throughout the site.
Site Admin

Site Admin

Super User has not set their biography yet

Posted by on in TAA Blog

TUGHE-1-min

Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya (TUGHE), mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Gaudence Kadyango aliyekuwa msimamizi wa uchaguzi wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya (TUGHE) tawi la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), akitoa maelezo kwa wapigaji kura kwenye uchaguzi mdogo wa tawi hilo uliofanyika leo kwenye ukumbi wa Transit uliopo Jengo la Kwanza la abiria(TBI).

 

TUGHE-2-min

Bw. Filbert Lyimo akijinadi katika nafasi ya Uenyekiti katika  uchaguzi mdogo wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya (TUGHE) tawi la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) uliofanyika leo katika ukumbi wa Transit uliopo jengo la kwanza la abiria (TBI).

 

TUGHE-3-min

Kaimu Mkurugenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Bw. Johannes Munanka (wa kwanza kulia), akifuatilia kwa makini zoezi la uchaguzi mdogo wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya (TUGHE) tawi la kiwanja hicho uliofanyika leo katika ukumbi wa Transit uliopo jengo la kwanza la abiria (TBI).

 

tughe-4-min

Wawakilishi wa wagombea wa nafasi ya Uenyekiti wa Chama  cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya (TUGHE) tawi la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), wakihesabu kura za nafasi ya Mwenyekiti mara baada ya uchaguzi uliofanyika katika Ukumbi wa Transit uliopo jengo la kwanza la abiria (TBI).

 

tughe-5-min

Wanachama wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya (TUGHE) tawi la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), wakihesabu kura za nafasi ya Uenyekiti Kamati ya Wanawake, katika uchaguzi uliofanyika kwenye ukumbi wa Transit wa Jengo la Kwanza la abiria (TBI).

 

TUGHE-6-min

Msimamizi wa uchaguzi mdogo wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya (TUGHE) tawi la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Bi. Honesta Ngowi kutoka Wizara ya Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana (kulia) akishughudia wanaohesabu kura za nafasi ya ujumbe wa TUGHE katika uchaguzi uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Jengo la Pili la abiria (TBII).

 

TUGHE-7-min

Wapiga kura katika uchaguzi mdogo wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya (TUGHE) tawi la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), wakimsikiliza Katibu wa tawi hilo, Bw. Thawabu Njeni akitoa ufafanuzi kabla ya kutangazwa kwa matokeo leo kwenye ukumbi wa mikutano wa Jengo la Pili la abiria (TBII).

Hits: 1274
0

DNIA-1-min

Kaimu Mkurugenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Bw. Johannes Munanka akiongea na wafanyakazi wa kiwanja hicho kwenye ukumbi wa mikutano wa Transit uliopo Jengo la Kwanza la abiria (TB1), ambapo walijadili masuala mbalimbali ya kiutendaji. Kulia ni Afisa Rasilimali Watu Mkuu Bi. Fatma Matimba.

 

DNIA-2-min

Wafanyakazi wa  Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), wakimsikiliza kwa makini Kaimu Mkurugenzi wa kiwanja hicho,  Bw. Johannes Munanka  alipokuwa akizungumza nao mambo mbalimbali ya kiutendaji.

 

DNIA-3-min

Meneja Uendeshaji wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA),  Bw. Vedastus Fabian (mwenye miwani mbele) akiandika mambo mbalimbali katika mkutano ulioitishwa na Kaimu Mkurugenzi wa JNIA, Bw. Johannes Munanka ambaye hayupo pichani.

 

DNIA-5-min

Afisa Uendeshaji wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Bi. Rachel Manyilizu akiuliza maswali kwa Kaimu Mkurugenzi wa JNIA (hayupo pichani) katika mkutano wa wafanyakazi uliofanyika kwenye ukumbi wa Transit katika jengo la Kwanza la abiria (TBI).

 

DNIA-6-min

Afisa Usalama, Bw. Musso John, akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali yaliyoulizwa katika mkutano ulioitishwa na Kaimu Mkurugenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Bw. Johannes Munanka uliofanyika kwenye ukumbi wa Transit uliopo katika Jengo la Kwanza la abiria (TBI).

 

DNIA-7-min

Fundi Umeme Mwandamizi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Bi Mastidia Ndyomulwango akiwasilisha hoja kwenye mkutano wa Wafanyakazi wa JNIA, ulioitishwa na Kaimu Mkurugenzi wake, Bw. Johannes kujadili masuala mbalimbali ya kiutendaji wa kazi.

 

DNIA-4-min

Kaimu Mkurugenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Bw. Johannes Munanka akijibu maswali ya wafanyakazi wa kiwanja hicho, alipokutana nao katika mkutano uiliofanyika katika ukumbi wa Transit uliopo Jengo la Kwanza la abiria (TBI).

Hits: 1153
0

Contact Us

Tel (Gen): +255 22 2842402/3
Fax: +255 22 2844495
Email: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.
P.O.Box 18000 Dar Es Salaam

Feedback & Enquires