Tanzania Airports Authority Blog

  • Home
    Home This is where you can find all the blog posts throughout the site.
Site Admin

Site Admin

Super User has not set their biography yet

image1Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) itatoa tuzo kwa viwanja vya ndege vitakavyofanya vizuri katika kutunza na kusimamia mazingira.

Hayo yalisemwa leo na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAA, Salim Msangi wakati wafanyakazi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania wakiadhimisha siku ya Mazingira Dunia kwa kufanya usafi nje ya kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) Dar es Salaam . TAA iliadhimisha Siku ya Mazingira Duniani kwa kufanya usafi (ambapo ilihusisha kyeka nyasi) na kuweka mbolea pamoja na kupunguza matawi ya miti iliyopandwa katika maadhimisho ya mwaka 2015.

Siku ya Mazingira Duniani itaadhimishwa kimataifa nchini Canada ikiongozwa na kaulimbiu ya "Connecting People to Nature", wakati kitaifa itafanyika mjini Butiama mkoani Mara ikiongozwa na kaulimbiu ya "Hifadhi ya Mazingira: Muhimili wa Tanzania ya Viwanda". Makamu wa Rais Samia Hassan Suluhu anatarajiwa kuwa mgeni rasmi wa maadhimisho haya.

Msangi aliwataka meneja wa viwanja vya ndege vilivyo chini ya usimamizi wa TAA nchini kutunza mazingara, ambapo aliahidi TAA kutoatuzo kwa kiwanja kitakachofanya vizuri zaidi.

Alisema kuwa wafanyakazi wa viwanja vya ndege wamekuwa mstari wa mbele kutunza mazingira miaka yote ili kuhakikisha jamii inaishi katika eneo salama.

Mbali na kufanya usafi wa kufyeka nje ya Terminal 3, pia wafanyakazi hao, waliweka mbolea na kupalilia miti waliyopanda mwaka 2015 katika eneo la VIP na pembeni mwa barabara ya kuelekea Kago (Cargo) . Vilevile matawi ya baadhi ya miti yalipunguzwa.

Kila mwaka wafanyakazi hao wa TAA wamekuwa wakishiriki katika maadhimisho hayo muhimu kwa kufanya shughuli mbalimbali kamavile kupanda miti, kufanya usafi n.k. katika maeneo tofauti tofauti.

Akifafanua kuhusu tuzo, Msangi alisema kuwa TAA itaanzisha tuzo ya kuhifadhi na kusimamia Mazingira (DG Environmental Award) na atakayeshinda atapewa tuzo hiyo itakayoshindaniwa na viwanja vyote vilivyo chini ya usimamizi wa TAA.

"Itaanzishwa tuzo na kiwanja kitakachoshinda, meneja wakiwanja hicho pamoja na wafanyakazi husika watazawadiwa tuzo na TAA ili kuhamasisha viwanja vingie navyo vifanye vizuri na kushinda kwenye maadhimisho yanayokuja, "alisema Msangi.

Kaimu Mkurugenzi wa TAA pia alizitaja shughuli zingine zinazofanywa na Mamlaka ili kutunza mazingira ni pamoja na kudhibiti maji taka yanayotoka viwajani, ambapo kuna mabwawa (oxidation ponds) yanayokusanya majitaka yote na kuyasafisha ili kukidhi viwango vilivyowekwa.

Mbali na kusafisha majitaka pia kuna mfumo (oil separator) wa kutenganisha maji na mafuta ili kulinda mazingira. Maji ya mvua yote yanayotoka katika eneo la maengesho ya ndege yameelekezwa katika mfumo huu ili kutenganisha maji na mafuta kabla ya kuyaruhusu kwenda kwenye mazingira.

Kupanda miti imekuwa ikipendezesha maneo na pia ikipunguza mrundikano wa gesi ukaa again, ambapo usafiri wa anga umekuwa ukichangia takribani 2% ya gesi ukaa (CO2) inayozalishwa dunia.

image2Mkuu wa Kitengo cha Mazingira, Jofta Timanywa alisema kuwa kila mwaka TAA imekuwa ikiadhimisha siku Siku ya Mazingira Duniani kwa kufanya kazi mbalimbali za kuhifadhi na kusimamia mazingira ikiwemo usafi maeneo mbalimbali pamoja na kupanda miti. 

 

 

 


image3

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Salim Msangi (kulia) na Kaimu Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa TAA, Mohamed Ally wakifanya usafi nje ya jengo la kuwasili na kuondokea abiria mashuhuri (VIP) leo wakati wafanyakazi wa mamlaka hiyo wakiadhimisha Siku ya Mazingira.

image4

Wafanyakazi wa TAA wakifanya usafi leo katika eneo la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (Terminal III)

image5

Wafanyakazi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) baada ya kumaliza kufanya usafi nje ya Kwanja wa Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) leo.

Hits: 1381
0

Mh. Waziri Mkuu, Kassim M. Majaliwa akiwasili kwenye kiwanja cha ndege cha Dodoma, na akipokelewa na Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mh. Prof. Makame Mbarawa.

Mh. Prof. Makame Mbarawa, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, akimtambulisha Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Mhandishi George Sambali kwa Mh. Waziri Mkuu, Kassim M. Majaliwa baada ya kuwasili kwenye kiwanja cha ndege cha Dodoma, kwa ajili ya kuweka jiwe la msingi katika mradi wa ukarabati na upanuzi wa kiwanja hicho.

Mh. Waziri Mkuu, Kassim M. Majaliwa akisalimiana na Meneja Msaidizi wa Mradi wa ukarabati na upanuzi wa kiwanja cha ndege cha Dodoma, Han Ying wa Kampuni ya China Henan International Cooperationm (CHICO), wanaofanya kazi hiyo.

Mh. Waziri Mkuu, Kassim M. Majaliwa akiweka jiwe la msingi la mradi wa ukarabati na upanuzi wa kiwanja cha ndege cha Dodoma, huku Mh. Prof. Makame Mbarawa, waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (watatu kutoka kushoto) akipiga makofi, pamoja na mkuu wa mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana (wa kwanza kulia).

Mh. Waziri Mkuu, Kassim M. Majaliwa akiwasha kitufe baada ya kuweka jiwe la msingi katika mradi wa ukarabati na upanuzi wa kiwanja cha ndege cha Dodoma, Julai 20, 2016.

Mh. Waziri Mkuu, Kassim M. Majaliwa akipiga makofi pamoja na wageni waalikwa katika sherehe za uwekaji jiwe la msingi katika mradi wa ukarabati na upanuzi wa kiwanja cha ndege cha Dodoma.

Msafara wa Mh. Waziri Mkuu, Kassim M. Majaliwa ukielekea kukagua mradi wa ukarabati na upanuzi wa kiwanja cha ndege Dodoma, ambapo barabara ya kuruka na kutua kwa ndege itawekwa tabaka jipya la lami lenye unene wa 100mm katika Kipande cha urefu wa mita 900 kwa upana wa mita 30.

Katibu Mkuu Uchukuzi, Leonard Chamuriho wa (pili kulia), akimweleza Mh. Waziri Mkuu, Kassim M. Majaliwa juu ya mradi wa ukarabati na upanuzi wa kiwanja cha ndege cha Dodoma, wakati Mh. Majaliwa akikagua mradi huo Julai 20, 2016.

Mh. Warizi Mkuu, Kassim M. Majaliwa (mwenye tai nyekundu) akiendelea kukagua mradi wa ukarabati na upanuzi wa kiwanja cha ndege cha Dodoma. Kulia mwenye mfuko mweusi, ni Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Mhandisi George Sambali.

Ukaguzi wa mradi wa ukarabati na upanuzi wa kiwanja cha ndege cha Dodoma ukiendelea.

Kazi ya ukarabati na upanuzi wa kiwanja cha ndege cha Dodoma ukiendelea.

Magari ya ujenzi yakiendelea na kazi katika mradi wa ukarabati na upanuzi wa kiwanja cha ndege cha Dodoma.

Mh. Waziri Mkuu, Kassim M. Majaliwa akihutubia wananchi wa mkoa wa Dodoma, katika sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi katika mradi wa ukarabati na upanuzi wa kiwanja cha ndege cha Dodoma.

Kamati ya mradi wa ukarabati na upanuzi wa kiwanja cha ndege cha Dodoma wakiwa katika picha ya pamoja na Mh. Waziri Mkuu, Kassim M. Majaliwa.

Wafanyakazi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), wakipiga picha ya pamoja na mgeni rasmi wa sherehe za kuweka jiwe la msingi katika mradi wa ukarabati na upanuzi wa kiwanja cha ndege cha Dodoma.

Wajenzi wa mradi wa ukarabati na upanuzi wa kiwanja cha ndege cha Dodoma, wa kampuni ya China Henan International Cooperation (CHICO) wakiwa katika picha ya pamoja na Mh. Waziri Mkuu, Kassim M. Majaliwa katika sherehe za kuweka jiwe la msingi la mradi huo.

Ndege ya shirika la ndege la Precision, ATR 72 5H-PWA ikitua kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma, Julai 21, 2016 baada ya njia kurefushwa, huku ikiwa imembeba Rais wa Zanzibar, Dr. Ali Mohamed Shein na ujumbe wake waliokuwa wakiudhuria mkutano mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM).

Precision Air, ATR 72 5H-PWA ikisogea kwenye maegesho baada ya kutua kwenye kiwanja cha Dodoma, ambacho barabara yake ya kutua na kupaa kwa ndege imeongezwa urefu kutoka mita 2 hadi mita 2.5.

Ndege ya shirika la ndege la Precision, ikiwa kwenye eneo la maegesho baada ya abiria waliotoka kwenye kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) kushuka, akiwemo Rais wa Zanzibar, Dr. Ali Mohamed Shein. MWISHO

Hits: 2244
0

Contact Us

Tel (Gen): +255 22 2842402/3
Fax: +255 22 2844495
Email: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.
P.O.Box 18000 Dar Es Salaam

Feedback & Enquires