Tanzania Airports Authority Blog

  • Home
    Home This is where you can find all the blog posts throughout the site.
Site Admin

Site Admin

Super User has not set their biography yet

Mh. Waziri Mkuu, Kassim M. Majaliwa akiwasili kwenye kiwanja cha ndege cha Dodoma, na akipokelewa na Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mh. Prof. Makame Mbarawa.

Mh. Prof. Makame Mbarawa, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, akimtambulisha Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Mhandishi George Sambali kwa Mh. Waziri Mkuu, Kassim M. Majaliwa baada ya kuwasili kwenye kiwanja cha ndege cha Dodoma, kwa ajili ya kuweka jiwe la msingi katika mradi wa ukarabati na upanuzi wa kiwanja hicho.

Mh. Waziri Mkuu, Kassim M. Majaliwa akisalimiana na Meneja Msaidizi wa Mradi wa ukarabati na upanuzi wa kiwanja cha ndege cha Dodoma, Han Ying wa Kampuni ya China Henan International Cooperationm (CHICO), wanaofanya kazi hiyo.

Mh. Waziri Mkuu, Kassim M. Majaliwa akiweka jiwe la msingi la mradi wa ukarabati na upanuzi wa kiwanja cha ndege cha Dodoma, huku Mh. Prof. Makame Mbarawa, waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (watatu kutoka kushoto) akipiga makofi, pamoja na mkuu wa mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana (wa kwanza kulia).

Mh. Waziri Mkuu, Kassim M. Majaliwa akiwasha kitufe baada ya kuweka jiwe la msingi katika mradi wa ukarabati na upanuzi wa kiwanja cha ndege cha Dodoma, Julai 20, 2016.

Mh. Waziri Mkuu, Kassim M. Majaliwa akipiga makofi pamoja na wageni waalikwa katika sherehe za uwekaji jiwe la msingi katika mradi wa ukarabati na upanuzi wa kiwanja cha ndege cha Dodoma.

Msafara wa Mh. Waziri Mkuu, Kassim M. Majaliwa ukielekea kukagua mradi wa ukarabati na upanuzi wa kiwanja cha ndege Dodoma, ambapo barabara ya kuruka na kutua kwa ndege itawekwa tabaka jipya la lami lenye unene wa 100mm katika Kipande cha urefu wa mita 900 kwa upana wa mita 30.

Katibu Mkuu Uchukuzi, Leonard Chamuriho wa (pili kulia), akimweleza Mh. Waziri Mkuu, Kassim M. Majaliwa juu ya mradi wa ukarabati na upanuzi wa kiwanja cha ndege cha Dodoma, wakati Mh. Majaliwa akikagua mradi huo Julai 20, 2016.

Mh. Warizi Mkuu, Kassim M. Majaliwa (mwenye tai nyekundu) akiendelea kukagua mradi wa ukarabati na upanuzi wa kiwanja cha ndege cha Dodoma. Kulia mwenye mfuko mweusi, ni Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Mhandisi George Sambali.

Ukaguzi wa mradi wa ukarabati na upanuzi wa kiwanja cha ndege cha Dodoma ukiendelea.

Kazi ya ukarabati na upanuzi wa kiwanja cha ndege cha Dodoma ukiendelea.

Magari ya ujenzi yakiendelea na kazi katika mradi wa ukarabati na upanuzi wa kiwanja cha ndege cha Dodoma.

Mh. Waziri Mkuu, Kassim M. Majaliwa akihutubia wananchi wa mkoa wa Dodoma, katika sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi katika mradi wa ukarabati na upanuzi wa kiwanja cha ndege cha Dodoma.

Kamati ya mradi wa ukarabati na upanuzi wa kiwanja cha ndege cha Dodoma wakiwa katika picha ya pamoja na Mh. Waziri Mkuu, Kassim M. Majaliwa.

Wafanyakazi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), wakipiga picha ya pamoja na mgeni rasmi wa sherehe za kuweka jiwe la msingi katika mradi wa ukarabati na upanuzi wa kiwanja cha ndege cha Dodoma.

Wajenzi wa mradi wa ukarabati na upanuzi wa kiwanja cha ndege cha Dodoma, wa kampuni ya China Henan International Cooperation (CHICO) wakiwa katika picha ya pamoja na Mh. Waziri Mkuu, Kassim M. Majaliwa katika sherehe za kuweka jiwe la msingi la mradi huo.

Ndege ya shirika la ndege la Precision, ATR 72 5H-PWA ikitua kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma, Julai 21, 2016 baada ya njia kurefushwa, huku ikiwa imembeba Rais wa Zanzibar, Dr. Ali Mohamed Shein na ujumbe wake waliokuwa wakiudhuria mkutano mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM).

Precision Air, ATR 72 5H-PWA ikisogea kwenye maegesho baada ya kutua kwenye kiwanja cha Dodoma, ambacho barabara yake ya kutua na kupaa kwa ndege imeongezwa urefu kutoka mita 2 hadi mita 2.5.

Ndege ya shirika la ndege la Precision, ikiwa kwenye eneo la maegesho baada ya abiria waliotoka kwenye kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) kushuka, akiwemo Rais wa Zanzibar, Dr. Ali Mohamed Shein. MWISHO

Hits: 2390
0

Posted by on in TAA Blog

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

Thea Semjela wa Uchukuzi SC akipeana mkono na mgeni rasmi Mwenyekiti TRAWU, Mussa Kalala kabla ya kukabidhiwa kombe la mshindi wa pili wa mchezo wa bao kwa wanawake katika michezo ya Mei Mosi.

Joyce Kumondi wa Ujenzi akipokea kombe la mshindi wa pili wa mchezo wa draft kwa wanawake, kutoka kwa mgeni rasmi wa mashindano ya Mei Mosi ,Mwenyekiti wa TRAWU, Mussa Kalala

Ally Zongo wa Uchukuzi SC akipokea kombe la mshindi wa tatu wa mchezo wa karata kwa wanaume, katika michuano ya Mei Mosi.

Mwanaisha Athuman wa Uchukuzi SC akipokea kombe la ubingwa wa netiboli kutoka kwa mgeni rasmi Mwenyekiti TRAWU, Mussa Kalala, katika mashindano ya Mei Mosi.

Wachezaji wa Uchukuzi SC wakiwa wamevipanga vikombe 11 walivyotwaa kwenye michezo mbalimbali ya Mei Mosi, iliyomalizika juzi mkoani Dodoma.

Bingwa wa baiskeli Chaptele Muhumba wa Uchukuzi SC akiwa amekumbatia kombe alilotwaa kwenye mashindano ya Mei Mosi.

Wachezaji na viongozi wa Uchukuzi SC wakishangilia baada ya kufanya vizuri kwenye mashindano ya Mei Mosi yaliyomalizika juzi mkoani Dodoma.

Wachezaji wa netiboli wa timu ya Uchukuzi SC wakishangilia baada ya kupokea kombe la ubingwa wa michezo ya Mei Mosi mkoani Dodoma. Uchukuzi waliwafunga Tamisemi kwa magoli 18-15.

Hits: 2431
0

Contact Us

Tel (Gen): +255 22 2842402/3
Fax: +255 22 2844495
Email: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.
P.O.Box 18000 Dar Es Salaam

Feedback & Enquires