Tanzania Airports Authority Blog

  • Home
    Home This is where you can find all the blog posts throughout the site.
Site Admin

Site Admin

Super User has not set their biography yet

Posted by on in TAA Blog

DNIA-min

Mkurugenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Bw. Paul Rwegasha akimwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongela katika michezo ya bonanza la uzinduzi wa mazoezi ya michezo ya Wizara, Idara na Taasisi za Serikali (SHIMIWI), lililofanyika leo kwenye viwanja vya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA).

 

25 08 2018 bonanza

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi), Mhandisi Dkt Leonard Chamuriho (aliyesimama) akizungumza na wanamichezo wa Sekta ya Uchukuzi walioshiriki leo kwenye bonanza la uzinduzi wa mazoezi ya michezo Wizara, Idara na Taasisi za Serikali (SHIMIWI) lililofanyika katika viwanja vya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA).

 

DSC 0362-min

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Bw. Hamza Johari (wa pili kulia) akiwa na Katibu  Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi), Mhandisi Dkt Leonard Chamuriho (wa tatu kushoto) akiwa katika bonanza la uzinduzi wa mazoezi ya michezo ya Wizara, Idara na Taasisis za Serikali (SHIMIWI), lililofanyika leo kwenye viwanja vya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA). Wa pili kushoto ni Mwenyekiti mpya wa Klabu ya Uchukuzi, Bw. Alphonce Mwingira.

 

DSC 0416-min

Timu ya wanawake ya kuvuta Kamba ya Uchukuzi wakivutana na wenzao ambao hawapo pichani katika bonanza la uzinduzi wa michezo ya Wizara, Idara na Taasisi za Serikali (SHIMIWI), lililofanyika leo kwenye Viwanja vya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA).

 

DSC 0419-min

Timu ya wanaume ya kuvuta Kamba ya Uchukuzi wakivutana na wenzao ambao hawapo pichani katika bonanza la uzinduzi wa michezo ya Wizara, Idara na Taasisi za Serikali (SHIMIWI) lililofanyika leo kwenye Viwanja wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA).

 

johari-min

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Bw. Hamza Johari (mbele namba 11) akiwafanyisha mazoezi watumishi kutoka taasisi mbalimbali zilizopo chini ya Sekta ya Uchukuzi, katika bonanza la uzinduzi wa mazoezi ya Wizara, Idara na Taasisi za Serikali (SHIMIWI), yaliyofanyika leo kwenye viwanja vya TCAA.  Wa kwanza kulia mbele ni Katibu Mkuu Sekta ya Uchukuzi, Mhandisi Dkt. Leonard Chamuriho.

Hits: 1427
0

Posted by on in TAA Blog

Simiyu 1-min

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (wa pili kushoto) jana akimsikiliza Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongela (watatu kushoto) alipotembelea banda la maonesho ya Kilimo na Sherehe za Nanenane la Mamlaka yanayofanyika kwenye uwanja wa Nyakabindi mkoani Simiyu.

 

simiyu 2-min

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongela (aliyenyoosha mkono) jana akimwonyesha chati yenye viwanja 58 vya ndege Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka alipotembelea banda la maonesho ya Kilimo na Sherehe za Nanenane la Mamlaka yanayofanyika kwenye uwanja wa Nyakabindi mkoani Simiyu.

 

simiyu3-min

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongela (wa kwanza kushoto) akimwelezea Mkuu wa Mkoa wa Simiyu mradi wa ujenzi wa kiwanja kipya cha Ndege cha mkoa huo kitakachojengwa eneo la Igegu, baada ya jana kutembelea banda la maonesho ya Kilimo na Sherehe za Nanenane yanayoendelea kwenye Uwanja wa Nyakabindi.

 

simiyu4-min

Mshauri wa Sera za Miundombinu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Bi. Pudencia (kushoto) jana akimsikiliza kwa makini Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongela akimweleza masuala mbalimbali alipotembelea banda la Maonesho ya Kilimo na Sherehe za Nanenane la Mamlaka yanayofanyika kwenye Uwanja wa Nyakabindi mkoani Simiyu.

 

simiyu5-min

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (katikati waliokaa) akiwa kwenye picha ya pamoja na Kamati ya maonesho ya Kilimo na Sherehe za Nanenane ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), jana alipotembelea banda la Mamlaka katika Uwanja wa Nyakabindi. Kulia waliokaa ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAA, Bw. Richard Mayongela.

 

simiyu6-min

Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Jumanne Sagini (wa pili kushoto) akipata taarifa ya ujenzi wa Kiwanja kipya cha Ndege cha mkoa huo kutoka kwa Mhandisi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Alex Kalumbete jana alipotembelea banda la maonesho ya Kilimo na Sherehe za Nanenane yanayofanyika kwenye Uwanja wa Nyakabindi.

 

simiyu7-min

Wafanyakazi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) wakiwa kwenye picha ya pamoja na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA),(mwenye suti nyeusi) jana alipotembelea banda lao la maonesho ya Kilimo na Sherehe za Nanenane yanayofanyika kwenye Uwanja wa Nyakabindi mkoani Simiyu.

 

simiyu8-min

Afisa Uhusiano wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Bw. Thomas Mushi (kushoto) akimweleza mambo mbalimbali Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongela (kulia) jana alipotembelea banda la maonesho ya Kilimo na Sherehe za Nanenane. Katikati ni Mkurugenzi wa Biashara na Masoko wa TTCL, Bw. Ally Mbega.

Hits: 1233
0

Contact Us

Tel (Gen): +255 22 2842402/3
Fax: +255 22 2844495
Email: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.
P.O.Box 18000 Dar Es Salaam

Feedback & Enquires