Tanzania Airports Authority Blog

  • Home
    Home This is where you can find all the blog posts throughout the site.

TAA Blog

This is our official blog. It contains different events which TAA participate director indirect. For more social aspect about TAA, please visit our blog from time to time. Thanks.

DSC 6549-min

Watendaji wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) kutoka Menejimenti na Vitengo vya Usalama, Uendeshaji na uzuiaji wanyamapori wakiwa katika mafunzo ndani ya Ukumbi wa watu Mashuhuri (VIP) katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA TB II).Walioketi mbele kushoto ni Meneja Rasilimali watu na Utawala Bw. Abdi Mkwizu kulia ni Mkurugenzi wa kituo cha Mafunzo ya Anga cha Kiwanja cha Ndege cha Incheon Bw. Chin Hyong, Ryu.

 

DSC 6544-min

Msimamizi Mwandamizi na Mkaguzi wa Usalama wa anga Bw. Sanghoom (Mark) Lim akitoa mafunzo kwa Watendaji wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) kutoka Menejimenti na Vitengo vya Usalama, Uendeshaji na uzuiaji wanyamapori kuhusu masuala ya Usalama katika Viwanja vya Ndege ndani ya Ukumbi wa watu Mashuhuri (VIP) katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA TB II).

 

DSC 6573-min

Meneja wa Mafunzo kutoka Kiwanja cha Ndege cha Incheoni Bi. Ji-Yoon Park akitoa mafunzo kwa Watendaji wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) kutoka Menejimenti na Vitengo vya Usalama, Uendeshaji na uzuiaji wanyamapori kuhusu namna ya kuandaa mpango wa kuwaongezea uwezo watendaji katika Viwanja vya Ndege. Mafunzo hayo yamefanyika ndani ya Ukumbi wa watu Mashuhuri (VIP) katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA TB).

Hits: 1917
0

01-min

Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa barabara TANROADS (aliesimama) Mhandisi Crispin Akoo akitoa taarifa ya Utekelezaji wa Mradi wa Jengo la 3 la abiria kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Prof.Adolph Mkenda alipotembelea Jengo hilo kuangalia namna ya kumuenzi Muasisi wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere.

 

02-min

Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Prof. Adolph Mkenda (tatu toka kulia) akisikiliza maelezo juu ya Mradi yanayotelewa na Mhandisi kutoka Wakala wa Barabara(TANROADS)Bi, Rehema Myeya alipofanya ziara hiyo mwishoni mwa wiki iliyopita.

 

03-min

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Bw, Richard Mayongela(pili kulia) akifanya majumuisho ya Ziara ya Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii na Uongozi wa Uhuru Media na Taasisisi zilizo chini ya Wizara hiyo mwishoni mwa wiki iliyopita.

Hits: 1894
0

Posted by on in TAA Blog

PICHA NO 1-min

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Bw, Richard Mayongela alipokuwa akifafanua jambo wakati wa Mkutano wa 22 wa Baraza Kuu la Wafanyakazi lililofanyika katika ukumbi wa LAPF Dodoma mapema leo.

 

PICHA NO 2-min

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe (tatu kushoto) katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya TAA (MAB) Mhandisi Prof. Ninatubu Lema (pili kushoto) Mkurugenzi Mkuu wa TAA Bw, Richard Mayongela (pili kulia) na Wajumbe mbalimbali mara baada ya kufungua Mkutano wa 22 wa Baraza Kuu la Wafanyakazi lililofanyika katika Ukumbi wa LAPF , Dodoma mapema leo.

 

PICHA NO 3-min

Wajumbe mbalimbali waliohudhuria Mkutano wa 22 wa Baraza Kuu la Wafanyakazi lililofanyika leo katika Ukumbi wa LAPF, Dodoma.

 

PICHA NO 4-min

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe alipokuwa akifungua rasmi Mkutano wa 22 wa Baraza Kuu la Wafanyakazi lililofanyika katika Ukumbi wa LAPF, Dodoma mapema leo.

 

PICHA NO 5-min

Kaimu Mkurugenzi wa Rasilimali watu na Utawala Bw, Lawrence Thobias alipokuwa akifafanua jambo wakati wa Mkutano wa 22 wa Baraza Kuu la Wafanyakazi lililofanyika leo katika Ukumbi wa LAPF, Dodoma.

 

PICHA NO 6-min

Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri (MAB) ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Mhandisi Prof. Ninatubu Lema alipokuwa akieleza jambo mara baada ya ufunguzi rasmi wa Mkutano wa 22 wa Baraza Kuu la Wafanyakazi lililofanyika katika Ukumbi wa LAPF, Dodoma mapema leo.

 

PICHA NO 7-min

Baadhi ya Viongozi Waandamizi wa Mamlaka wakifuatilia kwa umakini Hoja mbalimbali zilizokuwa zikijadiliwa katika Mkutano wa 22 wa Baraza Kuu la Wafanyakazi lililofanyika katika Ukumbi wa LAPF, Dodoma mapema leo.

 

PICHA NO 8-min

Mwenyekiti wa Mkutano ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania Bw, Richard Mayongela (katikati)alipokuwa akiongoza Mkutano wa 22 wa Baraza Kuu la Wafanyakazi lililofanyika katika Ukumbi wa LAPF, Dodoma mapema leo (toka kushoto) Bi Naomi Semadio Katibu wa baraza hilo, (toka kulia) bw, priscus mkawe katibu msaidizi wa baraza.

 

NO 9-min

Wajumbe mbalimbali wa Baraza Kuu la Wafanyakazi walipokuwa wakifuatilia kwa umakini hoja zilizokuwa mezani katika Mkutano wa 22 wa Baraza Kuu la Wafanyakazi lililofanyika katika Ukumbi wa LAPF, Dodoma

 

PICHA NO 10-min

Keki ya kuadhimisha kumbukumbu ya miaka 19 ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege tangu kuanzishwa na kuzinduliwa kwake tarehe 3 Desemba 1999.

Hits: 1747
0

PICHA 1-min

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja Vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Lawrence Thobias (Mwenye suti ya Kijivu) akisalimiana na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Afande Thobias Andengenye mara baada ya kuwasili katika jengo la Makao Makuu ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA) kwa ajili ya kikao Kazi na Makamanda wa Mikoa na Wakuu wa Vituo vya Zimamoto na Uokoaji Viwanja vya ndege Bara.

 

PICHA 2-min

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Afande Thobias Andengenye akizungumza na Makamanda wa Mikoa na Wakuu wa Vituo vya Zimamoto na Uokoaji Viwanja vya ndege Bara katika kikao kazi kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano Makao Makuu ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA) Banana Ukonga Jijini Dar es Salaam.

 

PICHA 3-min

Makamanda wa Mikoa na Wakuu wa Vituo vya Zimamoto na Uokoaji Viwanja vya ndege Bara Wakifuatilia Mada katika kikao kazi kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano Makao Makuu ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA).

 

PICHA 4-min

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja Vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Lawrence Thobias (Mwenye suti ya Kijivu) akijitambulisha katika kikao kazi kilichohusisha Makamanda wa Mikoa na Wakuu wa Vituo vya Zimamoto na Uokoaji Viwanja vya ndege Bara, kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano Makao Makuu ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA).

 

PICHA 8-min

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja Vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Lawrence Thobias (tatu kulia waliokaa), Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Afande Thobias Andengenye (katikati) na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu KADGO Mhandisi Martin Kanyamagoha wakiwa katika picha ya pamoja na Makamanda wa Mikoa na Wakuu wa Vituo vya Zimamoto na Uokoaji Viwanja vya ndege Bara, waliohudhuria katika kikao kazi kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano Makao Makuu ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA).

 

PICHA 10-min

Mkaguzi wa Viwanja Vya Ndege kutoka Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA) Bw. Burhan Hajji Majaliwa akitoa ufafanuzi juu ya swala la Ukaguzi wa Maofisa wa Usalama katika Viwanja vya Ndege katika kikao kazi kilichohusisha Makamanda wa Mikoa na Wakuu wa Vituo vya Zimamoto na Uokoaji Viwanja vya ndege Bara, kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano Makao Makuu ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA).

Hits: 1314
0

Posted by on in TAA Blog

DSC 1348-min

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongela (wa pili kushoto) leo akiongea na waandishi wa habari kuhusiana na shutuma za wizi wa pochi kwenye ukumbi wa mikutano wa Jengo la Pili la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA-TBII).

DSC 1355-min

Waandishi wa Habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari leo wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongela (katikati mbele) alipokuwa akiongea nao kuhusiana na shutuma za wizi wa pochi ndogo ya abiria (jina limehifadhiwa) aliyesafiri Septemba 8, 2018 kuelekea Dubai.

DSC 1357-min

Bw. Wael Hassan (kulia) akiushukuru uongozi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), mbele ya Waandishi wa Habari (hawapo pichani) kwa kuonesha picha zilizopigwa na kamera za Usalama za tukio la kulalamikiwa kwa wizi wa pochi ya dada yake (jina limehifadhiwa), aliyesafiri tarehe 8 Septemba, 2018 akielekea Dubai. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa TAA, Bw. Richard Mayongela.

Hits: 1262
0

Contact Us

Tel (Gen): +255 22 2842402/3
Fax: +255 22 2844495
Email: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.
P.O.Box 18000 Dar Es Salaam

Feedback & Enquires