DSC 6875-min

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania Bw, Richard Mayongela akifafanua jambo kabla ya kuweka saini mkataba wa makubaliano ya mafunzo kwa Watumishi wa TAA na Shirika linalotoa misaada la Korea (KOICA) leo katika Hoteli ya Hyatt Jijini Dar es salaam.

 

DSC 6883-min

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania Bw, Richard Mayongela akiweka saini katika mkataba wa makubaliano ya mafunzo ya miaka mitatu pamoja na Shirika la kutoa misaada la Korea Kusini, upande wa Tanzania (KOICA) huku akishuhudiwa na Mkurugenzi Mkaazi wa KOICA Bw, Joonsung Park leo katika Hotel ya Hyatt Jijini Dar es salaam.

 

DSC 6928-min

Mkurugenzi mkaazi wa KOICA Bw, Joonsung Park akitoa maelezo mafupi kabla ya kuweka saini mkataba wa makubaliano wa kutoa mafunzo kwa wafanyakazi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege leo katika Hotel ya Hyatt Jijini dar es salaam.

 

DSC 6903-min

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania Bw, Richard Mayongela (mwenye tai nyekundu kushoto), Mkurugenzi Mkaazi wa KOICA Bw, Joonsung Park (katikati) na Mkurugenzi wa Fedha na Utawala Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Zanzibar Bw, Muhidin Talib Abdullah Wakionyesha Mkataba Wa Makubaliano ya Mafunzo kwa Wafanyakazi mara baada ya kuweka saini katika Hotel ya Hyatt Jijini Dare Es Salaam mapema leo.