Tanzania Airports Authority Blog

  • Home
    Home This is where you can find all the blog posts throughout the site.

TAA YAKAMILISHA UHAKIKI WA VIWANJA 537.

Posted by on in TAA Blog
  • Font size: Larger Smaller
  • Hits: 1110
  • Subscribe to this entry
  • Print

MAMLAKA ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) ikishirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mkurugenzi wa Manispaa imekamilisha uhakiki wa viwanja 537 vilivyopo mitaa ya Luhanga na Kidole Kata ya Msongola vitakavyogawiwa kwa wananchi, kupisha upanuzi wa Kiwanja cha Ndege wa Kimataifa cha Julius Nyerere.

Kukamilika kwa uhakiki wa viwanja hivyo na kubainika kutokuwepo kwa kiwanja chochote chenye migogoro, hatua inayofuata ni kuvigawa viwanja hivyo kwa wananchi wote watakao athiriwa na upanuzi wa mradi huo hasa wakazi wa Kata za Kipunguni A na Kipunguni Mashariki.

Ukamilishaji wa kazi hiyo ndani ya wiki hii unafuatia agizo la Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye, alilolitoa Februari mwaka huu baada ya kufanya ziara katika Kiwanja cha Ndege wa Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) na kufanya mazungumzo na wananchi wa eneo hilo ya namna utaratibu utakaotumika kugawa viwanja hivyo.

Mhandisi Nditiye alisema ugawaji wa viwanja hivyo kwa wananchi hao utafanyika kwa awamu mbili ambapo awamu ya kwanza itahusu viwanja hivyo 537 ambavyo uhakiki wake umekamilika.
Alisema idadi ya wananchi watakaopisha mradi huo katika Kata ya Kipunguni A na Kipunguni Mashariki ni 1186 ambao watapatiwa viwanja kwa awamu mbili tofauti.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAA, Richard Mayongela, alisema viwanja hivyo vitaanza kugawiwa kwa wananchi 801 waliokubali kuhama huku wakisubiri kauli ya mahakama juu ya wananchi 326 waliokata rufani mahakamani kupinga agizo hilo, wananchi 59 tayari wamekwishapatiwa viwanja.

Mayongela alisema kwa mujibu wa tathmini ya mwaka 2013 wananchi hao wanadai fidia ya sh. bilioni 18.795 fedha ambazo Mamlaka inazitoa kwa awamu ili kufanikisha kuwaondoa wananchi hao kwa kuwapa viwanja na fedha taslimu.

Upatikanaji wa viwanja hivyo kwa ajili ya wanachi wa Kata ya Kipunguni A na Mashariki umetokana na mkataba wa utafutaji wa viwanja uliyoingiwa kati ya TAA na Kampuni ya Tanzania Remix iliyopewa kazi ya kutafuta viwanja 1600 vya wananchi watakaoathiriwa na kuhamishwa kutokana na mradi wa Upanuzi wa Kiwanja cha Ndege.

24 02 2018 TAA YAKAMILISHA UHAKIKI WA VIWANJA 537-01

Timu ya uhakiki ilipokuwa ikiendelea na zoezi mapema leo

24 02 2018 TAA YAKAMILISHA UHAKIKI WA VIWANJA 537-02

Timu ya uhakiki wa viwanja 537 ilipokuwa ikifanya majumuisho baada ya kukamilika kwa kazi hiyo leo

0

Contact Us

Tel (Gen): +255 22 2842402/3
Fax: +255 22 2844495
Email: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.
P.O.Box 18000 Dar Es Salaam

Feedback & Enquires