Simiyu 1-min

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (wa pili kushoto) jana akimsikiliza Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongela (watatu kushoto) alipotembelea banda la maonesho ya Kilimo na Sherehe za Nanenane la Mamlaka yanayofanyika kwenye uwanja wa Nyakabindi mkoani Simiyu.

 

simiyu 2-min

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongela (aliyenyoosha mkono) jana akimwonyesha chati yenye viwanja 58 vya ndege Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka alipotembelea banda la maonesho ya Kilimo na Sherehe za Nanenane la Mamlaka yanayofanyika kwenye uwanja wa Nyakabindi mkoani Simiyu.

 

simiyu3-min

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongela (wa kwanza kushoto) akimwelezea Mkuu wa Mkoa wa Simiyu mradi wa ujenzi wa kiwanja kipya cha Ndege cha mkoa huo kitakachojengwa eneo la Igegu, baada ya jana kutembelea banda la maonesho ya Kilimo na Sherehe za Nanenane yanayoendelea kwenye Uwanja wa Nyakabindi.

 

simiyu4-min

Mshauri wa Sera za Miundombinu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Bi. Pudencia (kushoto) jana akimsikiliza kwa makini Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongela akimweleza masuala mbalimbali alipotembelea banda la Maonesho ya Kilimo na Sherehe za Nanenane la Mamlaka yanayofanyika kwenye Uwanja wa Nyakabindi mkoani Simiyu.

 

simiyu5-min

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (katikati waliokaa) akiwa kwenye picha ya pamoja na Kamati ya maonesho ya Kilimo na Sherehe za Nanenane ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), jana alipotembelea banda la Mamlaka katika Uwanja wa Nyakabindi. Kulia waliokaa ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAA, Bw. Richard Mayongela.

 

simiyu6-min

Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Jumanne Sagini (wa pili kushoto) akipata taarifa ya ujenzi wa Kiwanja kipya cha Ndege cha mkoa huo kutoka kwa Mhandisi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Alex Kalumbete jana alipotembelea banda la maonesho ya Kilimo na Sherehe za Nanenane yanayofanyika kwenye Uwanja wa Nyakabindi.

 

simiyu7-min

Wafanyakazi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) wakiwa kwenye picha ya pamoja na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA),(mwenye suti nyeusi) jana alipotembelea banda lao la maonesho ya Kilimo na Sherehe za Nanenane yanayofanyika kwenye Uwanja wa Nyakabindi mkoani Simiyu.

 

simiyu8-min

Afisa Uhusiano wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Bw. Thomas Mushi (kushoto) akimweleza mambo mbalimbali Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongela (kulia) jana alipotembelea banda la maonesho ya Kilimo na Sherehe za Nanenane. Katikati ni Mkurugenzi wa Biashara na Masoko wa TTCL, Bw. Ally Mbega.